Thursday, June 2, 2016

LEO WEMBLEY NI ENGLAND vs PORTUGAL, RONALDO NJE! MECHI YA MWISHO KUJIPIMA EURO 2016.

LEO Uwanjani Wembley Jijini London England watacheza Mechi ya Kimataifa ya Kirafiki na Portugal ambayo itaingia kilingeni bila ya Nahodha wao Cristiano Ronaldo.
Portugal imeamua kuwapa mapumziko ya Wiki 1 Wachezaji wao wawili, Ronaldo na Pepe, ambao Jumamosi iliyopita waliichezea Real Madrid Fainali na kuibwaga Atletico Madrid huko San Siro, Milan Nchini Italy na kutwaa UEFA CHAMPIONS LIGI.
Pia Portugal itawakosa Bruno Alves na Nani ambao hivi karibuni waliichezea Klabu yao Fenerbahce kwenye Fainali ya Kombe la Uturuki na kufungwa 1-0 na Galatasaray.
Kwa upande wa England, Nahodha wao Wayne Rooney anatarajiwa kuanza Mechi hii baada ya Jumatano iliyopita kuingizwa Kipindi cha Pili na kufunga Bao la Pili wakati England ilipoichapa Australia 2-1.

Pia Straika toka kwa Mabingwa wa England Leicester City Jamie Vardy atacheza Mechi hii baada ya kuikosa ile na Australia aliporuhusiwa kwenda kufunga Ndoa.
Zote, England na Portugal, zimeshathibitisha Vikosi vyao vya Wachezaji 23 kwa UEFA kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya EURO 2016 zitakazoanza huko France hapo Juni 10.
Hivyo Mechi hii ya Leo ni muhimu kwa pande zote mbili kuimarisha Timu zao.
DONDOO MUHIMU:
-England imeishinda Portugal Mechi 1 tu katika 11 zilizopita, wakitoka Sare 8 na Kufungwa 2 katika hizo baada ya kuifunga Portugal Mechi 8 kati ya 11 ya kabla ya hapo ambazo walitoka Sare 2 na Kufungwa 1.
-Mechi za mwisho kati ya England na Portugal zote ziliamuliwa kwa Mikwaju ya Penati Tano Tano na zote Portugal kushinda, Penati 3-1 Kombe la Dunia 2006 na 6-5 EURO 2004.
ENGLAND - KIKOSI CHA WACHEZAJI 23:
MAKIPA:
Tom Heaton (Burnley), Fraser Forster (Southampton), Joe Hart (Manchester City)
MABEKI: Ryan Bertrand (Southampton), Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Liverpool), Danny Rose (Tottenham Hotspur), Chris Smalling (Manchester United), John Stones (Everton), Kyle Walker (Tottenham Hotspur)
VIUNGO: Dele Alli (Tottenham Hotspur), Ross Barkley (Everton), Eric Dier (Tottenham Hotspur), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), James Milner (Liverpool), Raheem Sterling (Manchester City), Jack Wilshere (Arsenal)
MAFOWADI: Harry Kane (Tottenham Hotspur), Daniel Sturridge (Liverpool), Jamie Vardy (Leicester City), Wayne Rooney (Manchester United), Marcus Rashford (Manchester United)
PORTUGAL - Kikosi cha Wachezaji 23:
MAKIPA: Rui Patricio (Sporting), Anthony Lopes (Lyon), Eduardo (Dinamo Zagreb)
MABEKI: Cedric Soares (Southampton), Vieirinha (Wolfsburg), Bruno Alves (Fenerbahce), Ricardo Carvalho (Monaco), Jose Fonte (Southampton), Pepe (Real Madrid), Eliseu (Benfica), Raphael Guerreiro (Lorient)
VIUNGO: Danilo Pereira (Porto), William Carvalho (Sporting), Adrien Silva (Sporting), Joao Mario (Sporting), Joao Moutinho (Monaco), Andre Gomes (Valencia), Renato Sanches (Benfica)
MAFOWADI: Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Nani (Fenerbahce), Eder (Lille - on loan from Swansea City), Ricardo Quaresma (Besiktas), Rafa Silva (Braga)