Sunday, June 12, 2016

EURO 2016: GERMANY 2 v 0 UKRAINE

Kwenye Mechi ya Pili ya Kundi C la EURO 2016 iliyochezwa Usiku huu huko Stade Pierre Mauroy Mjini Lille Nchini France, Mabingwa wa Dunia Germany waliibuka kidedea kwa ushindi wa Bao 1-0.
Awali Leo, katika Mechi nyingine ya Kundi C, Poland waliichapa Northern Ireland 1-0.
Germany walifunga Bao lao Dakika ya 19 kwa Kichwa cha Mustafi alieunganisha Frikiki ya Toni Kroos toka Winga ya Kulia.
Hadi Mapumziko Germany 1 Ukraine 0.
Dakika ya 89, Germany walimwingiza Nahodha wao Mkongwe Bastian Schweinsteiger ambae sasa yupo na Manchester United na ambae amekuwa nje ya Uwanja tangu Machi 20 akiuguza Goti na Dakika 1 baadae akaipa Germany Bao la Pili baada ya kaunta ataki safi iliyoishia kwa Krosi safi ya Mesut Ozil.