Monday, June 27, 2016

FULL TIME...ENGLAND 1 v 2 ICELAND, ROONEY NA WENZAKE HOI! WATUPWA NJE

WAKICHEZA huko Stade de Nice Mjini Nice Nchini France, Iceland Leo wameleta mtikisiko kwa kuibwaga England Bao 2-1 katika Mechi ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Kwenye Mechi hii, Kepteni wa England Wayne Rooney aliifikia Rekodi ya David Beckham ya kuichezea Mechi 115 akiwa Mtu wa Pili nyuma ya Kipa Peter Shilton ambae ameichezea England Mechi 125 na kuongoza kwa Mechi nyingi katika Historia ya England.

Na Rooney, ambae ndie Mfungaji Bora katika Historia ya England akiwa na Bao 53, aliipa England Bao la Kwanza kwa Penati katika Dakika ya 4 ambayo ilitolewa baada ya Raheem Sterling kuangushwa na Kipa Halldorsson.
Dakika 2 baadae Iceland wakasawazisha kutokana na Mpira wa kurushwa na kumkuta Ragnar Sigurdsson aliefunga.
Iceland wakapiga Bao lao la Pili Dakika ya 19 kwa shuti la Sigthorsson lililompenya Kipa Joe Hart kilaini.
Bao hizo zikadumu hadi Mechi inakwisha na Iceland kuitupa nje England na kusonga Robo Fainali ambapo watakutana na Wenyeji France.