Wednesday, June 8, 2016

MANCHESTER UNITED YAANZA KUTEMA CHECHE, YAMSAINI BEKI ERIC BAILLY

Manchester United wametangaza rasmi kumsaini Eric Bertrand Bailly ambae ameshakamilisha Uhamisho wake kutoka Villarreal CF na kinachosubiriwa ni kupata Kibali cha Kufanya Kazi huko Uingereza.
Bailly amesaini Mkataba wa Miaka Minne ambao una Kipengele cha kuongeza Miaka Miwili baada ya hapo.

Bailly, mwenye Miaka 22, aliichezea Villareal Mechi 47 tangu ajiunge nao Januari 29, 2015 na pia kuichezea Nchi yake Mara 15 akiwa sehemu ya Timu iliyotwaa Ubingwa wa Africa, AFCON 2015, akicheza Mechi zao zote za Fainali na kufunga moja ya Mikwaju ya Penati Tano Tano zilizoibwaga Ghana.

Akiongea baada ya kusaini Mkataba, Bailly alisema: “Ni ndoto iliyotimia kujiunga na Manchester United. Kucheza Soka la kiwango cha juu ndicho ninachotaka. Natka niendelee na naamini kufanya kazi na Jose Mourinho kutanisaidia kuendelea kwa njia sahii na Klabu sahihi.”

Nae Mourinho alizungumza: “Eric ni beki wa kati mwenye Umri mdogo na mwenye kipaji asilia. Ameendelea vizuri hadi Leo na ana uwezo kupanda zaidi!”