Sunday, June 5, 2016

MLIMBWENDE WA TAJI LA MISS ILEMELA 2016 APATIKANA


Mlimbwende Maria Frances (katikati) ametwaa taji la MISS ILEMELA 2016. Shindano la kumsaka mlimbwende huyo lilifanyika usiku wa jana June 04,2016 katika viunga vya Rock City Mall Jijini Mwanza.
Katika shindano hilo, nafasi ya pili imenyakuliwa na Mwanaisha Hija (kulia) huku nafasi ya tatu ikinyakuliwa na Happness Contantine (kushoto).

Miss Ilemela 2016, Maria Frances, akizungumza na BMG baada ya kutwaa taji hilo usiku wa kuamkia leo.

Miss Ilemela 2016 nambari mbili, Mwanaisha Hija, akizungumza na BMG baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo.

Miss Ilemela 2016 nambari tatu, Happness Contantine, akizungumza na BMG

Washiriki wa Miss Ilemela waliobahatika kuingia nafasi tano bora. Kulikuwa na washiriki 22

Washiriki wa Miss Ilemela 2016 wakipita jukwaani kwa madaha kabisa

Washiriki wa Miss Ilemela 2016, wakionyesha umahiri wa kucheza muziki

Majaji wa shindano la Miss Ilemela 2016

James Peter Chuwa, ambae ni Afisa Tarafa Ilemela, akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi Miss Ilemela 2016, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Manju Msambya.

Mchekeshaji Maganiko akichekesha jukwaani

Msanii chipukizi kutoka jijini Mwanza, G-Ricko akitoa burudani katika shindano la Miss Ilemela 2016

Msanii Nay Wa Mitego akitoa burudani katika shindano la Miss Ilemela 2016.