Monday, June 6, 2016

MO FARAH AVUNJA REKODI YA DAVE MOORCROFT

Mkimbiza upepo Mo Farah ameivunja rekodi ya mwingereza Dave Moorcroft iliyodumu kwa miaka 34 ya kukimbia mita elfu tatu kwa dakika saba sekunde 32 nukta saba tisa, sasa Mo Farah amezimaliza mbio hizo kwa dakika 7 sekunde thelathini na mbili na nukta sitini na mbili.
Ushindi wake huu ameutunuku kwa mwendazake, Mwanamasumbwi Mohamed Ali akisema alikuwa anampenda sana.