Saturday, June 4, 2016

MUHAMMAD ALI AFALIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 74

Muhammad Ali enzi za uhai wake.
Bondia bingwa wa zamani Muhammad Ali amefariki dunia jana Ijumaa akiwa kwenye Hospitali ya Phoniex alipokuwa akitibiwa tatizo la mfumo wa upumuaji. Muhammad Ali amefariki akiwa na umri wa miaka 74.
Bingwa huyo wa zamani wa uzito wa juu (World Heavyweight Champion) aliyeaminika kuwa mmoja kati ya mabondia bora zaidi kuwahi kutokea, Muhammad Ali maarufu kama “The Greatest” amefariki Dunia mapema leo katika hospitali ya Phoenix-area iliyopo Phoenix, Arizona alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Muhammad Ali alistaafu ndondi za kulipwa mwaka 1981 alipogundulika kuwa na ugojwa wa Parkinson (Parkinsons Disease) Mwaka 1984 na amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo hadi alipopatwa na mauti.
Mbali na ugonjwa huo pia Ali alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi pamoja na maambukizi katika njia ya mkojo.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi. Amina