Wednesday, June 15, 2016

RONALD KOEMAN MENEJA MPYA WA EVERTON

Klabu ya Everton imethibitisha usajili wa kocha Ronald Koeman kuwa mkufunzi wake mpya kwa kandarasi ya miaka mitatu.
Everton wamelipa dola milioni 5 kama fidia kwa mkufunzi huyo wa miaka 53 ambaye anaihama klabu ya Southampton baada ya kuisimamia kwa miaka miwili.
Everton imekuwa bila mkufunzi tangu ilipomtimua Roberto Martinez kabla ya mwisho wa msimu uliopita.

Koeman amesema kuwa Everton ni klabu yenye historia kubwa na ari ya kutaka kushinda huku mwenyekiti wa klabu hiyo akimwita raia huyo wa Uholanzi kama lengo lake la kwanza.