Thursday, June 2, 2016

RYAN GIGGS KUONDOKA MANCHESTER UNITED!

Ryan Giggs ataondoka Manchester United kabla Msimu ujao kuanza akiwania kuwa Meneja kwingineko.
Imedaiwa Meneja mpya wa Man United Jose Mourinho alitaka kumpa Giggs wadhifa wa kuwa mmoja wa Makocha wake lakini si Meneja Msaidizi cheo ambacho alikishikilia kwa Misimu Miwili chini ya Louis van Gaal.
Mourinho anataka Meneja Msaidizi awe Rui Faria ambae ndie msiri wake wa Siku nyingi.
Lakini inasemekana Giggs hataki ofa hiyo kwani hapendi kushushwa cheo na yuko tayari kuachia ngazi kwenye Klabu aliyodumu Miaka 29.
Pia zipo habari kuwa Klabu ya Man United inataka Giggs abaki na kuwa Kiungo wao kati ya Timu ya Vijana ya U-21 na Timu ya Kwanza.
Hivi sasa Giggs hayupo Manchester na yupo huko Dubai akila vakesheni akitarajiwa kurejea Wikiendi hii.
Mbali ya Rui Faria, Jopo la Ufundi la Mourinho ni pamoja na Silvinho Louro ambae ni Kocha wa Makipa pamoja na mtaalam mwingine Carlos Lalin.