Sunday, June 19, 2016

SIMBA YAMSAINI KIUNGO MOHAMED IBRAHIM TOKA MTIBWA

Simba imemsajili kiungo Mohamed Ibrahim kutoka klabu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa mkataba wa miaka miwili huku ada ya uhamisho wake ikiachwa kuwa siri.
Mohamed Ibrahim anakuwa mchezaji wanne kusajiliwa na Simba msimu huu akitanguliwa na Muzamir Yassin kutoka Mtibwa Sugar na wachezaji wengine wawili kutoka Mwadui FC Jamal Mnyate kutoka na Emanuel Semwanza.

Simba bado inamnyatia Shiza Kichuya kutoka Mtibwa Sugar lakini bado mazungumzo ya kuinasa saini yake yanaendelea.

Endapo Kichuya atatua Simba atakuwa ni mchezaji wa tatu kutoka Mtibwa kuhamia Simba msimu huu wakati Mtibwa itakuwa imeuza wachezaji wanne kwenda kwenye klabu za Simba na Yanga baada ya Andrew Vicent kusajiliwa Yanga mapema mwezi huu.