Saturday, June 4, 2016

WANA GUNNERS" WATUPIWA NENO KWAMBA MENEJA WAO WENGER HANG'OKI NG'OO EMIRATES!

MTENDAJI MKUU wa Klabu ta Arsenal Ivan Gazidis amesisitiza kuwa Meneja wao Arsene Wenger hataondoka Klabuni hapo.
Wenger atasherehekea Miaka 20 ya himaya yake kama Meneja wa Arsenal Mwezi Oktoba.
Lakini Mashabiki na Wadau wa Klabu hiyo wamechoshwa na Arsenal kuwa wasindikizaji kila Msimu bila kutwaa Taji na Msimu huu kulikuwa na presha kubwa kumtaka Wenger ang'oke baada ya kuanza Msimu vizuri kwenye mbio za Ubingwa wa Ligi Kuu England lakini kama kawaida yao matumaini yao kuyeyuka mwishoni.
Mara ya mwisho kwa Arsenal kutwaa Ubingwa wa England ni 2004 na baada ya hapo wametwaa FA CUP Mwaka 2014 na 2015.
Akielezea msimamo wa kumbakisha Wenger, Gazidis amesema: "Si mapenzi bali sababu ya Wenger kuwa Meneja wetu ni kuwa na imani ataleta mafanikio."

Hivi sasa Wenger yuko katika Mwaka wa mwisho wa Mkataba wake na hayajaanza mazungumzo na uamuzi wa nini kifuatie.