Sunday, June 19, 2016

YANGA YANASA MKALI MWINGINE TOKA ZIMBABWE

Mshambuliaji raia wa Zambia, Obrey Chirwa amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea klabu ya Yanga.
Chirwa ambaye alikuwa anaichezea FC Platinum ya Zimbabwe, amewasili jana Dar es Salaam na kukamilisha taratibu za usajili.
Yanga imekamilisha idadi ya wachezaji saba wa kimataifa kwa mujibu wa kanuni na sheria za TFF na nyongeza ya wachezaji watano kwa mijibu wa usajili wa CAF.
Nyota huyo anaungana na wachezaji wengine waliowahi kuichezea FC Platinum Donald Ngoma na Thaban Kamusoko ambao walisajiliwa msimu uliopita.
Klabu ya FC Platinum imethibitisha pia nyota huyo kujiunga na Yanga kwa kuandika ujumbe kwenye akaunti rasmi ya klabu hiyo uliosomeka: “Obreu Chirwa amejiunga rasmi na klabu ya Young Africans ya Tanzania kwa mkataba wa muda mrefu na kumtakia kila laheri kwenye safari yako mpya,”