Thursday, June 30, 2016

ZLATAN IBRAHIMOVIC HUYOO OLD TRAFFORD WIKIEND JULY 1, 2016

Zlatan Ibrahimovic anatarajiwa kukamilisha kabisa mpango wa kuhamia Manchester United kabla ya mwisho wa Wiki hii.
Ibrahimovic, mwenye Miaka 34, ni Mchezaji Huru baada ya kumaliza Mkataba wake na Paris St-Germain na anategemewa kusaini Mkataba wa Mwaka Mmoja na Man United.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Ibrahimovic kuchezea Klabu ya England baada ya kufanikiwa kutwaa Ubingwa akiwa na Klabu za Nchi 4 tofauti akibeba Mataji katika Misimu 13 toka Misimu 15 iliyopita.
Kwenye Msimu wake wa mwisho na PSG uliomalizika Mwezi Mei, Ibrahimovic aliibuka Mfungaji Bora wa Ligi 1 akipachika Bao 38.

Staa huyu atakuwa Mchezaji wa Pili kusainiwa na Meneja Mpya wa Man United, Jose Mourinho, baada ya kumsaini Eric Bailly kwa Pauni Milioni 30 kutoka Villarreal ya Spain huku pia Kiungo wa Borussia Dortmund, Henrikh Mkhitaryan, akisemwa yuko njiani nae kutua Man United.