Tuesday, June 21, 2016

ZLATAN IBRAHIMOVIC KUSTAAFU KUICHEZEA SWEDEN BAADA YA EURO 2016!

STRAIKA wa Sweden Zlatan Ibrahimovic ametangaza kustaafu kuichezea Timu ya Taifa ya Nchi yake mara baada ya EURO 2016.
Jumatano Sweden inaivaa Belgium katika Mechi yao ya mwisho ya Kundi E na Gemu hiyo inaweza kuwa ya mwisho kuichezea Nchi yake.
Ibrahimovic ameeleza: "Nasikia fahari kwa yote niliyofikia na Siku zote nitakuwa na Bendera ya Sweden!"
Manchester United inahusishwa sana kuwa ndio Klabu anayokwenda Straika huyo mwenye Miaka 34 baada ya kuwa Mchezaji huru kufuatia Mkataba wake na Paris St-Germain kumalizika mwishoni mwa Mwezi huu.

Ibrahimovic ameifungia Sweden Mabao 62 na hiyo ni Rekodi ya Bao nyingi kwa Taifa hilo na akiichezea Sweden kwenye Mechi ya Jumatano na Belgium itakuwa ni Mechi yake ya 116 akiwa Mechi 32 nyuma ya Mshika Rekodi Anders Svensson aliechezea Mechi 148.
Sweden watatupwa nje ya EURO 2016 ikiwa watashindwa kuifunga Belgium kwenye Mechi ya Kundi E lakini wakishinda watasonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16. 


Msimamo Kundi E: EURO 2016
Mechi za Mwisho za Makundi
Jumatano Juni 22

KUNDI F, Iceland v Austria (1900, Stade de France)
KUNDI F, Hungary v Portugal (1900, Stade de Lyon)
KUNDI E, Italy v Republic of Ireland (2200, Stade Pierre Mauroy)
KUNDI E, Sweden v Belgium (2200, Stade de Nice)