Wednesday, July 13, 2016

ANTONIO CONTE AWAFUA VIJANA WAKE CHELSEA KWA MARA YA KWANZA LEO COBHAM

Conte
MENEJA MPYA wa Chelsea ameanza himaya yake kwa kusisitiza John Terry anabaki kuwa Kepteni wa Timu hata kama hachezi.
Mwezi Mei, kukiwa na hatihati kuwa mwisho wa Terry umefika, Chelsea iliamua kumpa nyongeza ya Mwaka Mmoja baada ya Mkataba wake kwisha na hii ni mara ya 3 kupata nyongeza ya aina hiyo.
Terry, mwenye Miaka 35 na ambae ameichezea Chelsea zaidi ya Mechi 700, amekuwa akisuasua Msimu uliopita na Mwezi Januari aliwahi mwenyewe kutangaza kuwa anatarajia kuondoka mwishoni mwa Msimu.

Akiongea kwa mara ya kwanza na Wanahabari mara baada ya kutambulishwa rasmi hii Leo huko Stamford Bridge kama Meneja mpya, Antonio Conte, ambae aliteuliwa kuwa Meneja wa Chelsea Mwezi Aprili wakati bado akiwa Kocha wa Timu ya Taifa ya Italy na kupewa Mkataba wa Miaka Mitatu, amesema anamthamini sana John Terry.
Conte alieleza: “Ndio, John Terry ni Kepteni wa Chelsea acheze au asicheze. Daima ni Kepteni. Ni Mchezaji mzuri, mwenye haiba nzuri, na mvuto. Napenda kuongea nae kuhusu Klabu hii kwa sababu anaijua Klabu, ana moyo kuchezea Klabu hii na kwangu ni Mchezaji muhimu. Mchezaji akistahili kucheza, kwangu, atacheza tu!”
John Terry