Sunday, July 3, 2016

ARSENAL YATHIBITISHA KUMPATA TAKUMA

Arsenal wamethibitisha makubaliano ya kumsaini Straika wa Japan Takuma Asano kutoka Sanfrecce Hiroshima.
Mjapan huyo wa Miaka 21 sasa atapimwa afya yake na kupaswa kukidhi mahitaji mengine ya kisheria ili kukamilisha Uhamisho wake.
Takuma atakuwa Mchezaji wa Pili kusainiwa na Arsene Wenger hivi sasa na wa kwanza ni Kiungo wa Switzerland Granit Xhaka.
Kijana huyo wa Kijapani analetwa mahsusi kuziba pengo la Straika Danny Welbeck ambae atakuwa nje kwa Miezi kadhaa akiuguza Goti lake.
Takuma Asano alianza kuichezea Timu ya Taifa ya Japan Agosti Mwaka Jana na hadi sasa ameichezea Mechi 5.

Mchezaji huyu anakuwa Mjapan wa 3 kuichezea Arsenal chini ya Wenger wengine wakiwa ni Junichi Inamoto na Ryo Miyaichi.