Wednesday, July 13, 2016

ARSENE WENGER AMPIGA KISOGO THIERRY HENRY, SASA KUTIMKA ARSENAL!

Thierry Henry ataacha kuwa Kocha Klabuni Arsenal baada ya Arsene Wenger kuikataa ofa yake ya kufanya kazi ya Ukocha bure bila malipo.
Uamuzi huo unamfanya Henry, ambae ndie Mfungaji Bora Kihistoria Klabuni Arsenal, ajumuike na mlolongo mrefu wa Wachezaji wa zamani wa Klabu hiyo walionyimwa nafasi za kujiendeleza kwenye Ukocha.


Henry sasa anaungana na Patrick Vieira, Dennis Bergkamp, Marc Overmars na hivi karibuni, Mikel Arteta, kutokuwa na Wenger na Arsenal yake wakati wakijiendeleza kupata Vyeti vya juu vya Ukocha vya UEFA.

Baada ya kupata Leseni A ya Ukocha ya UEFA akifundisha Watoto Klabuni Arsenal, Henry alipaswa kufundisha Timu ya Wakubwa ili kupata Leseni ya UEFA ya Profeshenali na Mkuu wa Chuo cha Soka cha Arsenal, Andries Jonker, alimkubalia Henry kufundisha Kikosi chao cha U-18 lakini Wenger akapiga kikumbo Ofa hiyo.

Inasemekana Wenger alimwambia Henry kuwa kazi ya Ukocha wa Vijana wa U-18 ni kazi ya kudumu na haiwezi kuchanganywa na nyingine ambayo Henry huifanya kama Mchambuzi wa TV ya Sky Sports.
Ndipo Henry alipojitolea kufundisha bure lakini Wenger pia akakataa.
Vyanzo kutoka Arsenal vimedai Wenger hataki Mtu yeyote kuwa ndani ya Arsenal ambae baadae atakuwa tishio kwenye kibarua chake.

Pia, yapo madai kuwa Wenger alikerwa na kauli ya Mwaka Jana ya Henry akiwa kwenye Sky TV aliposema kuwa Mashabiki wa Arsenal hawana furaha na Wenger.