Saturday, July 2, 2016

BANGO KUBWA LASIMIKWA JIJINI MANCHESTER KUMLAKI ZLATAN IBRAHIMOVIC

Makaribisho ya Zlatan Old traffordBANGO kubwa limechomoza katikati ya Jiji la Manchester la kumkaribisha Staa wa Sweden Zlatan Ibrahimovic ambae yuko mbioni kukamilisha kujiunga kwake na Klabu ya Manchester United.
Bango hilo limesomeka: “MANCHESTER, INAMKARIBISHA ZLATAN” huku likionyesha Picha ya Straika huyo.
Cha kuvutia ni kuwa Bango hilo limesimikwa jirani tu na Duka la Manchester City wanalouza bidhaa za Klabu yao.
Tayari Ibrahimovic ameshatua Mchana huu huko Manchester baada ya kuletwa kwa Ndege maalum ya kukodi na yupo huko Kituo cha Mazoezi cha Man United, Carrington, akipimwa Afya yake.

Ibrahimovic, mwenye Miaka 34, tayari ameshaafikiana maslahi yake binafsi na Man United na atapewa Mkataba wa Mwaka Mmoja akiwa Mchezaji wa pili kusainiwa na Meneja Mpya Jose Mourinho.
Mchezaji wa kwanza kusainiwa na Mourinho ni Eric Bailly, Mchezaji wa Kimataifa wa Ivory Coast aliekuwa akichezea Villareal ya Spain.

Wakati huo huo, muda wowote kuanzia sasa Ndege nyingine ya kukodi inatarajiwa kutua Manchester kumfikisha Kiungo wa Borussia Dortmund ambae anatarajiwa kukamilisha Uhamisho wake kwenda Man United.