Monday, July 11, 2016

PORTUGAL MABINGWA UERO 2016, WAICHAPA 1-0 WENYEJI FRANCE LEO! EDER SHUJAA!


PORTUGAL wametwaa Ubingwa wa Ulaya baada kuwachapa Wenyeji wa Mashindano France 1-0 katika Fainali ya EURO 2016, iliyochezwa Stade de France Mjini Paris Nchini France.

Licha ya kumpoteza Mchezaji wao bora na Kepteni wao Cristiano Ronaldo katika Dakika ya 24 alipoumizwa na kulazimika kutoka, Portugal walihimili mashambulizi ya Wenyeji France na kwenda Sare 0-0 katika Dakika 90.

Dakika za Nyongeza 30 zikaja na Eder, aliengizwa Dakika ya 79 kumbadili Renato Sanchez, aliipa ushindi kwa Bao la Dakika ya 109 kwa Shuti la Mita 25 lililomshinda Kipa Hugo Lloris.

Huu ni ushindi wa kwanza kwa Portugal katika Mashindano makubwa na Kepteni Ronaldo kukabidhiwa Kombe la Ubingwa wa Ulaya.