Saturday, July 16, 2016

CAF CC: YANGA YATOSHANA NGUVU NA MEDEAMA YA GHANA KWA KUTOKA SARE YA 1-1

Mabingwa wa Tanzania Bara Yanga Leop wamejiweka nafasi ngumu mno kufuzu Nusu Fainali za KOMBE LA SHIRIKISHO, CAF CC baada ya kutoka Sare 1-1 na Medeama ya Ghana katika Mechi yao ya 3 ya Kundi A iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Sasa Yanga wamemaliza mzunguko wa kwanza wa Kundi A na bado wako mkiani mwa Kundi hilo wakiwa Pointi 1 tu baada ya kufungwa Mechi zao mbili za kwanza dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria na TP Mazembe zote kwa Bao 1-0.

Mechi hii iliyosimamiwa na Refa kutoka Egypt Nour El Din ilianza kwa Yanga kupata Bao Dakika ya Pili tu Mfungaji akiwa Mzimbabwe Donald Ngoma lakini Medeama walisawazisha Dakika ya 19 kwa Bao la Ofoni.

Mechi inayofuata kwa Yanga ni Julai 26 huko Ghana dhidi ya Medeama.