Saturday, July 2, 2016

CAF U-17: SEYCHELLES 0 vs 6 SERENGETI BOYS

TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Vijana chini ya Miaka 17, maarufu kama Serengeti Boys, Leo huko Mahe, Seychelles, imewanyuka wenzao wa Seychelles Bao 6-0 katika Mechi ya Marudiano ya Michuano ya CAF U-17 African Youth Championship na kusonga Raundi ya Pili kwa Jumla ya Bao 9-0.
Katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa Jijini Dar es Salaam hapo Juni 26, Serengeti Boys iliifunga Seychelles Bao 3-0 kwa Bao za Shaaban Zubeiry Ada, Ibrahim Abdallah Ali na Ally Hussein Msengi.
Leo, Wafungaji wa Serengeti Boys walikuwa ni Shaaban Zubeiry Dakika ya 7, Mohammed Abdalah, 49’, Hassan Juma, 47’ na 75’, Issa Makamba, kwa Penalti, 65’ na Yohana Nkomola, 90’.

Serengeti Boys, chini ya Makocha Bakari Shime na Kim Poulsen kutoka Denmark, sasa wataivaa South Africa katika Raundi ya Pili itakayochezwa baadae Mwezi huu.

Fainali za CAF U-17 zitachezwa Mwakani huko Madagascar na kushirikisha Nchi 8.