Thursday, July 21, 2016

CLAUDIO RANIERI ASISITIZA MAHREZ KUBAKI LEICESTER!

Claudio Ranieri amesisitiza kuwa Staa wake Riyad Mahrez atabakia Leicester City licha ya Arsenal kumuwania.
Baada ya Jana Mabingwa hao wa England kuwafunga Oxford Bao 2-1 katika Mechi ya kujipima nguvu, Ranieri alihojiwa na Wanahabari kuhusu tetesi za Riyad Mahrez kuhamia Arsenal na akagoma katakata kuwa haebdi popote.

Mahrez, Winga wa Kimataifa kutoka Algeria ambae Msimu uliopita aliisaidia sana kubeba Ubingwa wa England kwa mara ya kwanza huku yeye akizoa Tuzo ya PFA ya Mchezaji Bora wa Msimu, amehusishwa sana na kuhamia Klabu Vigogo huku Barcelona, Arsenal na Manchester City zikihusiswa nae.

Hivi karibuni, Leicester walifanikiwa kumbakiza Straika wao hatari Jamie Vardy alietakiwa na Arsene Wenger kuhamia Arsenal na kauli hii ya Ranieri ni pigo jingine kwa Wenger kwa kumkosa Mahrez.

Majuzi Leicester walimpoteza Kiungo wao stadi wa Kimataifa toka France, N’Golo Kante, aliehamia Chelsea, lakini Ranieri amesisitiza: “Kila Mtu hapa ana furaha. Nae Mahrez anataka kubaki. Hakuna Mchezaji mwingine ataondoka. Tutabaki wote pamoja!”

Kwenye Mechi yao ya Jana, Oxford walitangulia kufunga kwa Frikiki ya Chris Maguire lakini Leicester wakapiga Bao 2 kupitia Demarai Gray na Jeffrey Schlupp.

Kwenye Mechi hii, Ranieri aliwachezesha kwa mara ya kwanza Wachezaji wao wapya Ron-Robert Zieler, Luis Hernandez na Ahmed Musa na pia kuwatumia Chipukizi kutoka Chuo chao cha Soka, Admiral Muskwe na Hamza Choudhury.