Saturday, July 2, 2016

CRYSTAL PALACE YASAINI WACHEZAJI WAWILI KWA MPIGO

KLABU ya Ligi Kuu England Crystal Palace Jana ilisaini Wachezaji Wawili kwa mpigo.
Winga wa Newcastle anaechezea England, Andros Townsend, amenunuliwa na Crystal Palace kwa Pauni Milioni 13 kutoka Newcastle na Kipa wa France, Steve Mandanda, anaedakia Marseille nae amechukuliwa kwa Dau ambalo halikutajwa.

Townsend, mwenye Miaka 24, aliichezea Newcastle kwa Miezi 6 tu na kufunga Bao 4 katika Mechi 13 baada ya kuhamia hapo kutoka Tottenham Mwezi Januari 2016.
Winga huyo amesaini Mkataba wa Miaka Mitano na Palace huku Fowadi Dwight Gayle aakienda Newcastle.
Nae Kipa wa France, Steve Mandanda mwenye Miaka 31, ametua Palace kutoka Marseille ya France ambako alicheza Mechi 443 katika Misimu 9 na sasa amesaini Mkataba wa Miaka Mitatu na Palace.
Mandanda ametwaa Ubingwa wa France mara 1 na Kombe la Ligi la France mara 3 huko Marseille.
Kipa huyu anakuwa Kipa wa 7 kutoka France kudakia Klabu za Ligi Kuu England ambayo pia inae Kipa Nambari Wani wa France, Hugo Lloris, anaedakia Tottenham Hotspur.

Hivi sasa Mandanda yupo pamoja na Lloris kwenye Timu ya Taifa ya France ambayo Jumapili itacheza Mechi ya Robo Fainali ya EURO 2016 itakayochezwa huko Stade de France, Paris, Nchini France.