Saturday, July 23, 2016

DAVID MOYES ATUA SUNDERLAND LEO, MSIMU MPYA 2016/17 SASA KUWA PATASHIKA!

David MoyesSunderland imemteua David Moyes kuwa Meneja mpya wa Sunderland kwa Mkataba wa Miaka Minne.

Moyes, aliewahi kuwa Meneja wa Everton na Manchester United, anambadili Sam Allardyce, maarufu kama Big Sam, ambae sasa ndie Meneja mpya wa Timu ya Taifa ya England.

Uteuzi huu wa Moyes umethibitishwa na Tovuti ya Klabu ya Sunderland ambapo Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Ellis Short, ametoa Taarifa.

Nae Moyes ametoa shukran zake kwa kupewa nafasi huko Sunderland ambayo imekuja baada ya kufukuzwa huko Man United na baadae huko Spain alipokuwa na Timu ya Real Sociedad.

Kabla ya hapo, aliiongoza vizuri Timu ya Everton kwa Miaka 11 na hasa hilo kumfanya Mwenyekiti wa Sunderland Ellis Short kumteua.

Sunderland itaanza Msimu mpya wa Ligi Kuu England hapo Agosti 13 kwa kucheza Ugenini na Man City.