Saturday, July 2, 2016

DORTMUND YATHIBITISHA HENRIKH MKHITARYAN KUJIUNGA NA MAN UNITED

BORUSSIA DORTMUND imethibitisha kuwa Henrikh Mkhitaryan atajiunga na Manchester United.
Kwa mujibu wa Taarifa yao waliyoitoa kwenye Tovuti yao, Klabu hiyo imethibitisha kuwa baada ya Mazungumzo mazito Mkhitaryan, mwenye Miaka 27, atahamia Old Trafford.

Mkuu wa Dortmund, Hans-Joachim Watzke, ametamka kuwa wamepokea Ofa nzuri kutoka kwa Man United na hivyo wameamua kuikubali kwani baada ya Mwaka mmoja Mchezaji huyo wa Kimataifa kutoka Armenia angeweza kuondoka bure bila kulipwa senti.
Staa huyo alikuwa amebakiza Mwaka Mmoja tu kwenye Mkataba wake.
Inaaminika Dau la Uhamisho la Mkhitaryan ni Pauni Milioni 23.6 na anakuwa Mchezaji wa 3 kujiunga na Man United chini ya Meneja Mpya Jose Mourinho katika kipindi hiki.
Wengine waliosainiwa na Man United ni Eric Bailly na Zlatan Ibrahimovic.
Msimu uliopita, Mkhitarayn aliifungia Dortmund Bao 18.