Friday, July 1, 2016

EURO 2016: WALES WAINYUKA BELGIUM, SASA KUIVAA PORTUGAL NUSU FAINALI!

WALES wametinga Nusu Fainali baada ya kutoka nyuma kwa Bao Moja na kuichapa Belgium 3-1 huko Stade Pierre Mauroy, Lille, Nchini France, katika Mechi ya Robo Fainali ya EURO 2016, Mashindano ya Mataifa ya Ulaya,
Belgium walitangulia kufunga katika Dakika ya 13 kwa Shuti kali la Radja Nainggolan la Mita 30.
Wales walisawazisha Dakika ya 30 baada ya Kona ya Ramsey kuunganishwa kwa Kichwa na Ashley Williams.
Bao hizo zilidumu hadi Mapumziko.

Wales walipata Bao lao la Pili Dakika ya 55 baada ya robson-Kanu kuwahadaa Mabeki kadhaa wa Belgium na kugeuka na kujikuta yuko uso kwa uso na Kipa Thibaut Courtois ambapo alifunga kwa Shuti la pembeni.
Wales waliongoza 3-1 katika Dakika ya 85 kufuatia Krosi ya Gunter kuunganishwa kwa Kichwa na Sam Vokes alieingizwa Kipindi cha Pili kumbadili Robson-Kanu.

Hadi Mechi inakwisha, Wales 3 Belgium 1.
Wales sasa watacheza na Portugal kwenye Nusu Fainali ambayo itachezwa Jumatano Julai 6 huko Stade de Lyon Mjini Lyon Nchini France
.