Friday, July 8, 2016

FAINALI EURO 2016: CLATTENBURG KUPULIZA KIPENGA FRANCE v PORTUGAL JUMAPILI STADE DE FRANCE MJINI PARIS.

UEFA imemteua Refa Mark Clattenburg kuchezesha Fainali ya Mashindano ya Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, itakayochezwa Stade de France Mjini Paris Nchini France kati ya Wenyeji France na Portugal hapo Jumapili.
Wiki 6 zilizopita, Clatternburg, Refa kutoka Uingereza, ndie aliechezesha Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI huko San Siro, Milan, Italy ambayo Real Madrid iliibwaga Atletico Madrid na kutwaa Ubingwa wa Ulaya.
Pia, Clattenburg, mwenye Miaka 41, ndie aliechezesha Fainali ya FA CUP huko Wembley, London hapo Mei 21 wakati Manchester United ikiifunga Crystal Palace 2-1.
Portugal na France zilitinga Fainali hii ya EURO 2016 kwa Portugal kuifunga Wales 2-0 na Jana France kuichapa Germany 2-0.

Hii Fainali ya EURO 2016 Clattenburg atasaidiwa na Simon Beck na Jake Collin huku Wasaidizi wa Nyongeza wakiwa Anthony Taylor na Andre Marriner.