Saturday, July 30, 2016

FULL TIME: ARSENAL 2 v 1 MLS ALL-STARS, DROGBA AITUNGUA TENA GUNNERS!

ARSENAL wameshinda Mechi yao ya Kirafiki huko San Jose, California Nchini Marekani walipowachapa Kombaini ya Mastaa wanaocheza Ligi ya huko, MLS All Stars 2-1.
Kwa mara nyingine tena, Didier Drogba aliwatoboa Arsenal kwa kuipiga Bao lake la 16 katika Mechi zake 16 dhidi yao tangu awe huko England na Chelsea.

Arsenal ndio walitangulia kufunga katika Dakika ya 11 kwa Bao la Penati ya Joel Campbell iliyotolewa baada ya yeye kuangushwa na Laurent Ciman lakini Didier Drogba kusawazisha Dakika ya 45.

MLS All Stars, mbali ya kuwa na Didier Drogba, walikuwa na Maveterani wengine kina Kaka, Andrea Pirlo na Clint Dempsey, waliwasumbua sana Arsenal ambao walicheza bila ya Nyota wao Olivier Giroud, Aaron Ramsey, Laurent Koscielny na Mesut Ozil.

Arsenal walipiga Bao lao la ushindi Dakika ya 87 kupitia Chuba Akpom.
Mechi inayofuata kwa Arsenal ni Jumatatu watakapocheza na Klabu ya Mexico Chivas de Guadalajara.

Arsenal wataanza Kampeni yao ya Ligi Kuu England huko Emirates hapo Agosti 14 dhidi ya Liverpool.

VIKOSI:
Arsenal (Mfumo 4-2-3-1):
Cech; Debuchy (Bellerin 46), Holding (Martinez 67), Bielik (Chambers 46), Gibbs (Monreal 46); Elneny (Willock 67), Coquelin (Xhaka 46): Oxlade-Chamberlain (Zelalem 67), Wilshere (Iwobi 46), Campbell (Adelaide 67); Walcott (Akpom 67)

MLS All-Stars (Mfumo 4-2-3-1): Blake; Rosenberry, Ciman, Van Damme, Acosta (Vincent 56), Pirlo (Kjestan 32), Beckerman (Farrell 45), dos Santos (Trapp 45), Kaka (Giovinco 45), Villa, (Piatti 33), Drogba (Bingham 45).