Wednesday, July 6, 2016

GERARDO MARTINO NAE AJIUZULU ARGENTINA

Gerardo Martino amejiuzulu kama Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Argentina akimfuata Kepteni wa Timu hiyo Lionel Messi ambae nae alistaafu kuichezea mara baada ya Timu yao kushindwa Fainali ya Copa America huko USA walipobwagwa kwa Penati na Chile.

Martino, mwenye Miaka 53 na ambae ni maarufu kwa Jina la ‘Tata’, aliteuliwa kuwa Kocha wa Argentina mara baada ya Argentina kufungwa Fainali ya Kombe la Dunia la Mwaka 2014 na kumrithi Alejandro Sabella.

Martino alishinda Mechi 19 katika ya 29 huku Sare zikiwa 7 na Kufungwa 3 katika Mechi alizoisimamia Argentina.

Kujiuzulu kwa Martino kumethibitishwa na AFA, Chama cha Soka cha Argentina.
Hili ni pigo jingine kwa Soka la Argentina kufuatia kustaa kwa Messi, mwenye Miaka 29, ambae ameichezea Nchi yake Mechi 113 na kufunga Bao 55.