Thursday, July 21, 2016

GUARDIOLA AANZA VIBAYA NA CITY YAKE , AKUBALI KICHAPO CHA BAO 1-0 KUTOKA KWA BAYERN MUNICH!

Wakisalimiana marafikiCarlo Ancerlott
PEP GUARDIOLA ameanza utawala wake Manchester City kwa kufungwa 1-0 katika Mechi ya Kirafiki huko Allianz Arena Jijini Munich Nchini Germany mikononi mwa Bayern Munich ambayo ndiyo Klabu yake aliyotokea.
Bayern, ambayo iliweka Bango la kumkaribisha Guardiola kwenye Geti la kuingilia Uwanjani, ilifunga Bao lao la ushindi Dakika ya 76 baada ya Shuti la Erdal Ozturk kumbabatiza Gael Clichy na kumhadaa Kipa Angus Gunn.
Akichezesha Kikosi mchanganyiko, Guardiola aliwatumia Matineja Watano huku Mafulbeki wake Wawili, Pablo Maffeo na Angelino Tasende, wakiwa na Miaka 18 kila mmoja wakishirikiana pamoja na Mkongwe Aleksandar Kolarov.
Kipindi cha Pili, Guardiola aliimarisha Kikosi chake kwa kuwaingiza Wilfried Bony, Fabian Delph, Gael Clichy na Yaya Toure lakini Bayern, chini ya Meneja Mpya Carlo Ancelotti aliemrithi Guardiola, ndio waliibuka kidedea.
VIKOSI VILIVYOANZA:
Man City: Caballero; Maffeo, Adarabioyo, Kolarov, Angelino; Fernandinho, Fernando, Zinchenko; Barker, Iheanacho, Navas.
Bayern: Ulreich; Rafinha, Martinez, Alaba, Bernat; Alonso, Feldhahn, Lahm; Ribery, Benko, Green.Mchezaji wa Bayern akishangilia bao