Friday, July 8, 2016

JOSE MOURINHO NA BENCHI LAKE LA UFUNDI, RUI FARIA NDIE ATAKUWA MENEJA MSAIDIZI WAKE.

IMETHIBITISHWA kwamba mshirika na msiri wa Siku nyingi wa Jose Mourinho Rui Faria ndie atakuwa Meneja Msaidizi wa Manchester United chini ya Meneja huyo mpya huko Old Trafford.
Cheo hicho kilikuwa kikishikiliwa na Ryan Giggs aliekishika chini ya Mameneja waliotimuliwa David Moyes na Louis van Gaal.
Faria amekuwa pamoja na Jose Mourinho tangu huko Barcelona Mwaka 1996 wakienda pamoja kila Klabu aliyoenda Mourinho tangu wakati huo.
Wengine kwenye Benchi la Ufundi la Man United chini ya Jose Mourinho ni Silvino Louro ambae alianza kama Kocha wa Makipa, Ricardo Formosinho, Carlos Lalin, Emilio Alvarez na mchunguzi Giovanni Cerra.
Timu hiyo ya Mourinho ndio imepewa jukumu la kuifufua Man United na kuifanya iwemo kwenye mbio za Ligi Kuu England kitu ambacho wamekikosa tangu astaafu Sir Alex Ferguson Mwaka 2013.
Msimu uliopita Man United ilimaliza Nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu England na kukosa nafasi ya kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao wa 2016/17 na sasa watacheza UEFA EUROPA LIGI kuanzia Hatua ya Makundi.