Thursday, July 21, 2016

JULEN LOPETEGUI AGOTE NDIE KOCHA MPYA SPAIN

Shirikisho la Soka la Spain RFEF, Leo limethibitisha kuwa Julen Lopetegui Agote ndie Kocha mpya wa Timu ya Taifa ya Spain.

Lopetegui, ambae anakaribia kutimiza Miaka 50, alikuwa kwenye mlolongo wa Watu ambao walikuwemo kwenye mchakato wa kumrithi Vicente del Bosque aliestaafu Julai 4 mara baada ya Spain kutupwa nje ya EURO 2016B na kupoteza Taji lao la Ubingwa wa Ulaya.

Kocha huyu mpya ambae enzi zake za Uchezaji alikuwa Kipa amewahi kuzifundisha Timu za Taifa za Vijana za Spain za U-19 na U-20 kati ya Mwaka 2010 na 2012 na ile ya U-21 kati ya 2012 na 2014.


Akiwa na U-19 Mwaka 2012 na U-21 Mwaka 2013, Lopetegui alitwaa Ubingwa wa Ulaya akiwa na Chipukizi ambao sasa ni maarufu, Alvaro Morata na Thiago Alcantara.