Friday, July 8, 2016

KIPA PETR CECH ASTAAFU SOKA YA KIMATAIFA

Mlinda lango wa Arsenal Petr Cech ambaye ni raia wa Jamhuri ya Czech ametangaza kuwa amestaafu katika soka ya kimataifa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 ndiye mchezaji aliyelichezea sana taifa lake kupitia mechi 121 alizoshirikia tangu aanze mwaka 2002.
Alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha Czech ambacho kilifika nusu fainali ya Euro2004 kabla ya kushindwa na mabingwa Ugiriki.

''Nilipokuwa mtoto,ndoto yangu ilikuwa kuchezea timu ya taifa hata japo mara moja,aliuambia mtandao wa Arsenal.''Baada ya kushiriki mara nyingi naona fahari'',alisema Cech.