Monday, July 11, 2016

KLABU YA WEST HAM UNITED YAMSAJILI GOKHAN TORE


West Ham imemsaini Winga wa Besiktas Gokhan Tore kwa Mkopo wa Mwaka Mmoja ukiwa na kipengele cha kumbeba kwa Mkataba wa kudumu.
Tore, ambae ni Fowadi wa Turkey aliezaliwa Germany, alikuwa na Chelsea kwenye Timu ya Vijana kwa Miaka Miwili na kwenda kucheza huko Besiktas chini ya Meneja wa sasa wa West Ham Slaven Bilic.
Msimu uliopita, Tore alifunga Bao 4 na kutengeneza 6 katika Mechi 24 akiisaidia Besiktas kuipiku Fenerbahce na kutwaa Ubingwa wa Uturuki kwa zaidi ya Pointi 5.
Tore ametoboa kuwa Bilic ndie aliemfanya ahamie West Ham.