Wednesday, July 13, 2016

KLOPP NA BALOTELLI WAPISHANA, AAMBIWA TAFUTA KLABU NYINGINE!

MENEJA wa Liverpool Jurgen Klopp amemwambia Straika wao Mario Balotelli atafute Klabu nyingine.
Balotelli, mwenye Miaka 25, alikuwa huko kwao Italy Msimu uliopita akichezea AC Milan lakini hivi sasa amerejea Liverpool akiwa Mazoezini kujitayarisha kwa Msimu mpya.

Lakini Mchezaji huyo, aliejiunga na Liverpool Mwaka 2014 na kufunga Bao 4 tu, anaonekana sasa hafai na hilo Klopp amepasua.
Meneja huyo Mjerumani amesema: “Hajafikia kiwango cha kuweza kugombea Nafasi moja au mbili na Wachezaji Wanne au Watano. Lazima tupate suluhisho na itatokea Klabu inayomtaka Balotelli mpya.”

Akiwa na AC Milan Msimu uliopita, Balotelli alifunga Bao 3 tu katika Mechi 23 na kuachwa Timu ya Taifa ya Italy iliyocheza Fainali za EURO 2016 ambazo zilikwisha Jumapili iliyopita.