Thursday, July 28, 2016

KOCHA PEP GUARDIOLA APATA USHINDI WAKE WA KWANZA AKIWA NA MAN CITY


Kocha Pep Guardiola amepata ushindi wake wa kwanza akiwa na Manchester City baada ya kufikia hatua ya penati dhidi ya Borussia Dortmund katika mchezo uliochezwa nchini China.

Kipa wa Manchester City Angus Gunn, 20, aliokoa penati ya Mikel Morino na kuihakikishia ushindi wa penati 6-5 baada ya mchezo kuishia kwa sare ya 1-1 huko Shenzhen katika dimba la Longgang.

Katika mchezo huo mchezaji wa Dortmund Christian Pulisic, 17, alisawazisha katika dakika za mwisho, na kufanya matokeo kuwa moja kwa moja baada ya awali Sergio Aguero kuifungia goli la kwanza la mchezo huo.


Kipa wa Manchester City Angus Gunn akipangua penati iliyoipa ushindi timu yake

Wachezaji wa Manchester City wakifurahia ushindi baada ya kipa Gunn kupangua penati