Sunday, July 3, 2016

LEICESTER YAMSAINI KIUNGO NAMPALYS MENDY

MABINGWA wa England Leicester City wamemsaini Kiungo wa France Nampalys Mendy kutoka Nice wakati Arsenal wakithibitisha makubaliano ya kumsaini Straika wa Japan Takuma Asano. 
Nampalys Mendy, mwenye Miaka 24 ambae aliwahi kucheza chini ya Claudio Ranieri walipokuwa wote Monaco na kupanda Daraja kuingia Ligi 1 huko France, amesaini Mkataba wa Miaka Minne huko Leicester City na kuungana tena na Ranieri.
Mendy alijiunga na Nice Mwaka 2013 na kuichezea Mechi za Ligi 110.

Mfaransa huyu anakuwa Mchezaji wa Tatu kusainiwa na Ranieri katika kipindi hiki na wengine ni Kipa Ron-Robert Zielerand na Beki Luis Hernandez.
Mendy ameichezea Timu ya Taifa ya France ya Vijana chini ya Miaka 21 mara 5.