Friday, July 22, 2016

LEO HII IJUMAA MCHANA: MAN UNITED vs BORUSSIA DORTMUND, SHANGHAI, CHINA

MANCHESTER United wanaanza ziara yao huko China, rasmi kama Tour 2016, presented by Aon, kwa kucheza na Wababe wa Germany Borussia Dortmund huko Shanghai Stadium Mjini Shanghai Ijumaa Saa 9 Mchana kwa saa za hapa Tanzania

Hii ni Mechi ya Pili kwa Meneja mpya wa Man United ambae Juzi alianza kwa kuichapa 2-0 Wigan huko DW Stadium, England.

Lakini hii ni Mechi ngumu kwani Dortmund wameanza matayarisho yao ya Msimu Wiki kadhaa nyuma na kucheza Mechi 5 za kujipima wakati Man United ndio kwanza wameanza tu.

Mvuto kwa Mechi hii ni Mchezaji mpya wa Man United, Henrikh Mkhitaryan, kuivaa Klabu yake ya zamani aliyoihama rasmi hivi karibuni.
Pia, Chipukizi wa Man United, Adnan Januzaj, anaweza kukumbana na Timu ambayo Msimu uliopita aliichezea kwa Mkopo.
Nae Mchezaji wa zamani wa Man United alieondoka Mwaka 2014, Shinji Kagawa, alienunuliwa toka Dortmund anaweza pia kucheza kuiwakilisha Dortmund dhidi ya Man United.

Hivi sasa Dortmund wapo chini ya Kocha Thomas Tuchel aliechukua wadhifa Mwaka 2015 kutoka kwa Jurgen Klopp ambae sasa yupo England na Liverpool.

Kwa Dortmund, tegemeo lao kubwa ni Straika kutoka Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang, ambae Msimu uliopita alipachika Bao 39 katika Mechi 46 na kupitwa tu katika Ufungaji Bora huko Germany na Straika wa Poland anaecheza kwa Mabingwa Bayern Munich Robert Lewandowski.

Man United na Dortmund zimekutana mara 6 na zote ni kwenye michuano rasmi ya UEFA na mara ya mwisho ni kwenye Nusu Fainali za UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 1997 ambazo Dortmund walishinda Mechi zote 2 kwa Bao 1-0 wakielekea kutwaa Ubingwa wa Ulaya.

Lakini, kati ya hizo Mechi 6, Man United wameitwanga Dortmund mara 3 na kipigo cha mwisho ni 4-0 walichoshinda Old Trafford Mwaka 1964 kwenye Inter-Cities Fairs Cup.

MAN UNITED - KIKOSI KAMILI HUKO CHINA:
De Gea, Romero, Johnstone, Bailly, Blind, Fosu-Mensah, Jones, McNair, Rojo, Shaw, Smalling, Tuanzebe, Valencia, Carrick, Herrera, Januzaj, Lingard, Mata, Memphis, Mkhitaryan, A. Pereira, Young, Keane, Rashford, Rooney.

Ratiba/Matokeo:
Julai 2016

16 Jul Kirafiki: Wigan Athletic 2 - 0
22 Jul Ziara 2016: Borussia Dortmund [China, Saa 9 Mchana]
25 Jul Ziara 2016: Manchester City [China, Saa 8 na Nusu Mchana]
30 Jul Ziara 2016: Galatasaray [Sweden, Saa 2 na Nusu Usiku]

Agosti 2016
03 Aug Wayne Rooney Mechi Maalum: Everton [Old Trafford, Saa 4 Usiku]
07 Aug FA Community Shield: Leicester City [Wembley, Saa 12 Jioni]

Ligi Kuu England
14 Aug: Bournemouth [Ugenini, Saa 9 na Nusu Mchana]
19 Aug: Southampton [Old Trafford, Saa 4 Usiku]
27 Aug: Hull City [Ugenini, Saa 1 na Nusu Usiku]

Septemba 2016
10 Sep: Manchester City [Old Trafford, Saa 8 na Nusu Mchana]
18 Sep: Watford [Ugenini, Saa 8 Mchana]
24 Sep Premier League Leicester City [Old Trafford, Saa 8 na Nusu Mchana]