Monday, July 25, 2016

LEO JUMATATU: MANCHESTER CITY vs MANCHESTER UNITED

DABI ya Manchester itahamia huko Beijing National Stadium Mjini Beijing Nchini China Jumatatu Saa Nane na Nusu Mchana wakati Manchester City watakapoikwaa Manchester United kwenye Mechi ya Kirafiki.

Mbali ya kuwa ni Mechi kati ya Mahasimu wakubwa huko England, Mechi hii pia inawakutanisha wapinzani wawili wakiongoza Timu zao za England na kukutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza.
Wapinzani hao ni Meneja Mpya wa City Pep Guardiola na Meneja Mpya wa Man United Jose Mourinho ambao walijijengea uhasama mkubwa kati yao walipokuwa huko Spain wakiziongoza Real Madrid na Barcelona.
Kwenye Mechi hii, Man United wanatarajiwa kuvaa Jezi zao mpya za Nyumbani za Msimu mpya wa 2016/17 zilizotengenezwa na Adadis.Kila Timu inatarajiwa kutumia Wachezaji tofauti ili kutoa mazoezo kwa Vikosi vyao kamili.

Hii itakuwa Mechi ya Pili kwa kila Timu za majaribioa kwa ajili ya Msimu mpya ambapo wote walifungwa katika Mechi za za kwanza.

City walichapwa 1-0 na Bayern Munich wakati Man United ikifungwa 4-1 na Borussia Dortmund.

Kihistoria Man United wako mbele ya City katika Mechi zao 171 walizocheza kati yao kwa kushinda Mechi 71 dhidi ya 49 za City.

Kwenye Mechi yao ya mwisho waliyokutana huko Etihad Stadium Mwezi Machi, Marcus Rashford ndie aliefunga Bao la ushindi na kuwapa Man United ushindi.