Wednesday, July 6, 2016

LIONEL MESSI NA BABAYE WAHUKUMIWA JELA MIEZI 21, WAPANGA KUKATA RUFAA!

NYOTA wa Barcelona Lionel Messi amehukumiwa Kifungo cha Miezi 21 Jela kwa kosa ka ukwepaji Kodi huko Spain lakini huenda akanusurika kwenda Jela.
Messi na Baba yake Mzazi, Jorge Messi, wamehukumiwa Kifungo hicho hicho lakini kwa mujibu wa Sheria za Spain Kifungo chochote cha chini ya Miaka Miwili kinaweza kuwa Kifungo cha Nje bila ya kukitumikia Gerezani.

Mahakama huko Jijini Barcelona imewatia hatiani Messi na Baba yake kwa Makosa Matatu ya Ukwepaji Kodi lakini wanaweza kwenda Mahakama ya juu kukata Rufaa.

Vile Vile Mahakama imeamua Messi alipe Faini ya Pauni Milioni 1.7 na Baba yake kutozwa Faini ya Pauni Milioni 1.27.

Wawili hao walionekana kuwa na hatia ya kuikosesha Spain Kodi ya kiasi Pauni Milioni 3.19 kati ya Miaka ya 2007 na 2009.

Wakati wa Kesi hiyo, Messi alijitetea kuwa yeye alikuwa hajui chochote kuhusu mambo yake ya Kifedha kwani yeye alicheza Mpira tu.