Thursday, July 7, 2016

EURO 2016: GERMANY 0 v 2 FRANCE, ANTOINE GRIEZMANN AWAPELEKA FRANCE FANALI SASA KUKUTANA NA MUZIKI WA PORTUGAL!


WENYEJI France wa Mashindano ya Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, Leo wamewamwaga Mabingwa wa Dunia Germany katika Nusu Fainali ya pili iliyochezwa huko Stade Velodrome Mjini Marseille na kutinga Fainali kucheza na Portugal

Licha ya Germany kutawala Kipindi cha Kwanza, France walipata Bao lao kwa Penati pale Refa wa Italy Nicola Rizzoli alipoamua Bastian Schweinsteiger ameunawa Mpira wa Kona akijaribu kuokoa Kichwa cha Patrice Evra.

Penati hiyo ilipigwa na kufungwa na Antoine Griezmann katika Dakika ya 47 ya Kipindi cha Kwanza.
Hadi Mapumziko Wenyeji France 1 Mabingwa wa Dunia Germany 0. Germany waliendelea kutawala lakini wakapigwa Bao la Pili Dakika ya 72 kufuatia ufundi mkubwa wa Paul Pogba na Antoine Griezmann kuudonyoa na kutinga wavuni.
France watacheza Fainali na Portugal ambayo Jumatano iliifunga Wales 2-0 katika Nusu Fainali ya Kwanza.
Mpaka muda wa mapumziko wa dakika 45 kipindi cha kwanza Germany 0 v 1 France, bao la France likifungwa na Antoine Griezmann kwa mkwaju wa penati dakika ya 45. Mshindi hapa anasonga Fainali na atakwaana na Portugal walioifunga bao 2-0 Wales jana. Fuattilia kwa karibu bukobasports.com kwa Michezo hii ya Euro 2016.
VIKOSI:
GERMANY:
Neuer, Kimmich, Boateng, Howedes, Hector; Kroos, Can, Schweinsteiger; Muller, Ozil, Draxler
Akiba: Leno, Mustafi, Khedira, Schurrle, Podolski, Weigl, Tah, Gotze, Sane, Gomez, Ter Stegen

FRANCE: Lloris, Sagna, Koscielny, Umtiti, Evra; Pogba, Matuidi; Sissoko, Griezmann, Payet; Giroud
Akiba: Mandanda, Jallet, Rami, Kante, Cabaye, Gignac, Martial, Schneiderlin, Mangala, Digne, Coman, Costil
Refa: Nicola Rizzoli (Italy)