Sunday, July 31, 2016

MABINGWA ENGLAND LEICESTER CITY WATWANGWA 4-0 NA PSG!

MABINGWA wa England Leicester City Leo hii wamepigwa Bao 4-0 na Mabingwa wa France Paris St-Germain huko Stubhub Center, Carson, California kwenye moja ya michuano ya International Champions Cup.
Hadi Mapumziko PSG walikuwa mbele 2-0 kwa Bao za Penati ya Dakika ya 26 ya Edinson Cavani na lile la Dakika ya 45 la Jonathan Ikone.
Kipindi cha Pili waliongeza Bao 2 kupitia Lucas Moura, Dakika ya 64, na Odsonne Edouard, Dakika ya 90.
Mechi inayofuata kwa Leicester ni Jumatano huko Stockholm, Sweden ambako watacheza na Mabingwa wa Spain FC Barcelona.
Jumapili Agosti 7, Leicester watajimwaga Wembley Jijini London kucheza Machi ya kufungua pazia Msimu mpya wa England kwa kugombea Ngao ya Jamii dhidi ya Mabingwa wa FA.CUP Manchester United.

VIKOSI VILIVYOANZA:
LEICESTER (Mfumo 4-4-2):
Schmeichel, Hernandez, Huth, Morgan, Chillwell, Mahrez, Mendy, Amartey, Schlupp, Uloa, Okazaki
PSG (Mfumo 4-5-1): Areola, Meunier, Luiz, Kimpembe, Maxwell, Di Maria, Pastore, Motta, Stambouli, Ikone, Cavani
REFA: Ismail Elfath