Tuesday, July 5, 2016

MABINGWA LEICESTER CITY WAMPATA AHMED MUSA

MABINGWA wa Ligi Kuu England Leicester City wamekubaliana na CSKA Moscow ya Urusi ili kumsaini Fowadi wa Nigeria Ahmed Musa.
Mchezaji huyo wa Miaka 23 alisaini CSKA Mwaka 2012 na kuifungia Bao 54 katika Mechi 168.

Huku Kocha wa CSKA Leonid Slutsky akikiri kumpoteza Musa, Mchezaji huyo natarajiwa Jumatano kupimwa afya yake huko Leicester.

Musa, alieanza kuichezea Timu ya Taifa ya Nigeria Mwaka 2010, ameifungia Timu hiyo Bao 11 katika Mechi 58.