Friday, July 8, 2016

MABINGWA LEICESTER CITY WAMSAINI AHMED MUSA

MABINGWA wa England Leicester City wametangaza rasmi kumsaini Ahmed Musa kutoka CSKA Moscow kwa Dau ambalo halikutajwa na Uhamisho huu utakamilika baada ya kupatikana kwa Cheti cha Uhamisho wa Kimataifa.

Musa, mwenye Miaka 23 na ni Mchezaji wa Kimataifa wa Nigeria, aliifungia CSKA ya Urusi Bao 13 katika Mechi 30 za Ligi Msimu uliopita na anakuwa Mchezaji wa 4 kusainiwa na Leicester katika kipindi hiki.

Wachezaji wengine wapya waliosainiwa na Meneja Claudio Ranieri hivi sasa ni Nampalys Mendy, Ron-Robert Zieler na Luis Hernandez.