Saturday, July 30, 2016

MAN UNITED UGENINI ULLEVI KUCHEZA LEO DHIDI YA GALATASARAY. ZLATAN NDANI

Manchester United Jumamosi wapo huko Ullevi Stadium Mjini Gothenburg Nchini Sweden kucheza Mechi ya Kirafiki na Galatasaray ya Uturuki huku Mchezaji wao mpya Zlatan Ibrahimovic akitarajiwa kucheza Mechi yake ya kwanza.
Zlatan Ibrahimovic, ambae ni Mchezaji wa Kimataifa wa Sweden, anatarajiwa kuwepo Kikosini pamoja na wapya wenzake Eric Bailly na Henrikh Mkhitaryan.

Wengine ambao huenda wakacheza kwa mara ya kwanza kwenye Mechi za kujiandaa kwa Msimu mpya ni pamoja na Kepteni Wayne Rooney, Anthony Martial na Morgan Schneiderlin ambao walipewa Mapumziko zaidi baada ya kuchezea Nchi zao kwenye Fainali za Euro 2016 huko France Mwezi Juni na mapema Julai.

MAN UNITED - KIKOSI KAMILI HUKO SWEDEN:
De Gea, Johnstone, Romero, Bailly, Blind, Darmian, Jones, Rojo, Shaw, Valencia, Carrick, Fellaini, Herrera, Lingard, Mata, Mkhitaryan, Schneiderlin, Young, Ibrahimovic, Martial, Memphis, Rashford, Rooney
http://i2.mirror.co.uk/incoming/article8519667.ece/ALTERNATES/s615b/Ullevi-pitch.jpg