Monday, July 4, 2016

MANCHESTER CITY WAKAMILISHA USAJILI WA OLEKSANDR ZINCHENKO KUTOKA FC UFA YA RUSSIA


Oleksandr Zinchenko Kutoka FC Ufa kwenye Ligi ya premia ya Russian ambaye kwa sasa ana miaka 19.
Manchester City imemsaini Kiungo wa Miaka 19 kutoka Ukraine Oleksandr Zinchenko ambae anachezea Klabu ya FC Ufa.
Kijana huyo anaichezea Timu ya Taifa ya Ukraine na hivi Juzi alikuwemo kwenye Timu hiyo iliyocheza Mechi za Kundi C la EURO 2016 huko France na kufungwa Mechi zao zote 3 dhidi ya Germany, Northern Ireland na Poland.

Zinchenko anakuwa Mchezaji wa 4 kusainiwa na City hivi sasa chini ya Bosi Mpya Pep Guardiola na wengine ni Ilkay Gundogan, Aaron Mooy na Nolito.