Friday, July 8, 2016

MARCELO BIELSA AJIUZULU SIKU MBILI BAADA YA KUPEWA TIMU YA LAZIO!

Marcelo Bielsa.
MENEJA wa Lazio, Marcelo Bielsa amejiuzulu wadhifa wake huo ikiwa zimepita siku mbili toka klabu hiyo imeteue kushikilia nafasi hiyo. Klabu hiyo ilithibitisha Juzi kuwa kocha huyo wa zamani wa Chile, alikuwa amekubali kuchukua kibarua cha kuinoa timu hiyo na kutoa taarifa rasmi za uteuzi wake, hata hivyo Bielsa ameonekana kubadili uamuzi wake. Lazio ilithibitisha kocha huyo mwenye umri wa miaka 60 na jopo lake la ufundi wangetua jijini Rome kesho kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya lakini suala hilo linaonekana kutowezekana tena. Mshambuliaji wa zamani, kocha wa Primavera na aliyekuwa kocha wa muda msimu uliopita, Simone Inzaghi anatarajiwa kupewa kibarua cha muda wakati Roma ikitafuta kocha mwingine wa kudumu.