Friday, July 8, 2016

MECKY MAXIME MENEJA MPYA KAGERA SUGAR, ASAINI MWAKA MMOJA!

Baada ya tetesi za muda mrefu, hatimaye Mecky Maxime ametua Kagera Sugar. Maxime ambaye alikuwa akiinoa Mtibwa Sugar, sasa amesaini mkataba wa kuinoa Kagera Sugar. Meneja wa Kagera Sugar, Mohammed Hussein amesema Maxime ndiye kocha mkuu akichukua nafasi ya Adolf Rishard.
Awali, kulikuwa na taarifa za kuondoka kwa Maxime kwenda Kagera, lakini uongozi wa Mtibwa Sugar ulilikataa hilo. Kuna tarifa Mtibwa Sugar inatarajia kumrejesha Salum Mayanga ambaye sasa anainoa Prisons.