Tuesday, July 5, 2016

MIDDLESBROUGH YAMSAJILI MARTEN DE ROON LEO

Klabu iliyopanda Daraja, Middlesbrough, imemsaini Kiungo wa Atalanta Marten de Roon kwa Ada ambayo haikutajwa lakini inakisiwa kuwa ni Pauni Milioni 12.

Kiungo huyo kutoka Netherlands alifunga Bao 1 katika Ligi ya Italy Serie A Msimu uliopita.

Huyu anakuwa Mchezaji wa Tatu kusainiwa na Boro katika kipindi hiki na wengine ni Bernardo Espinosa kutoka Sporting na Winga waAjax, Viktor Fischer.