Monday, July 4, 2016

MOURINHO ATAMBULISHWA RASMI MENEJA MAN UNITED, ASEMA ‘ROONEY ATAMCHEZESHA KIVINGINE’

LEO huko old Trafford Jijini Manchester, Jose Mourinho ametambulishwa rasmi kama Meneja Mpya wa Manchester United na kisha kuongea na Wanahabari.

Mourinho ameieleza kazi ya Meneja Man United ndiyo kazi ambayo kila Mtu anaitaka.

Alisema: “Mara mbili nimefika Nchi hii. Lakini safari hii ni tofauti. Ni ngumu kuelezea. Ni ngumu kuielezea Klabu hii. Hii si kazi ya ndoto yangu, huu ni ukweli. Mimi ni Meneja wa Manchester United. Hii ni kazi ambayo kila Mtu anaitaka.”
Akiwageukia Mashabiki, Mourinho alieleza: “Najua wajibu, najua matarajio. Nafahamu urithi wake. Nafahamu nani wako nyuma yangu, naifahamu historia ya Klabu. Najua nini Mashabiki wanatumai. Changamoto hii hainipi mchecheto kutokana na historia yangu ya Miaka 10 iliyopita.”
Alipohojiwa kama kuna kitu anataka aonyeshe Watu kwamba bado yuko thabiti, Mourinho alijibu: “Kuna Mameneja hawajatwaa Ubingwa kwa Miaka 10. Wengine hawajawahi. Mie nilitwaa Ubingwa Mwaka Mmoja tu uliopita! Ikiwa mimi nataka kuonyesha kitu, je hao?”

Tangu kwa Mourinho kuteuliwa kuwa Meneja baada ya kufukuzwa Louis van Gaal Mwezi Mei, Man United imewasajili Wachezaji Wapya Wawili, Zlatan Ibrahimovic na Beki wa Ivory Coast Eric Bailly huku Kiungo wa Borussia Dortmund Henrikh Mkhitaryan akiwa njiani kuthibitishwa.

Pia Kiungo wa France na Juventus PaulPogba akitajwa sana.

Mourinho amesema: “Tuliamua kulenga Wachezaji Wanne. Mpaka tumpate huyo wan ne tutafanya bidi. Mchezaji wa 3 atakuwa rasmi hivi karibuni.”

Kuhusu Kepreni Wayne Rooney, Mourinho alieleza: “Pengine sasa sio Straika tena, pengine sio Namba 9 tena lakini kwangu hawezi kuwa Namba 6 au Mtu wa kucheza Mita 50 toka Golini. Ndio, pasi zake ni za ajabu lakini hata mie, bila presha, pasi zangu za ajabu. Kutumbukiza Mpira wavuni ndio kazi ngumu kuipata. Kwangu mimi, atakuwa Namba 9 au 10 au 9 na nusu lakini 6. Hawezi kuwa hata 8!”